
Natamani Kukusahau
Author: Shamte Kilalile
Baada ya uhusiano kuvunjika, mwanamziki wa covers anakabiliana na maumivu ya mapenzi, wapenzi wake wa zamani na mama mtoto wake mwenye kumchafua kwenye mitandao ya kijamii. Ni stori kwa kizazi hiki ambacho kila kitu kwenye mitandao ya kijamii. Kama ni mpenzi wa filamu za musical, utaipenda stori hii.
Keywords for this book
You can only order 1 ebook at a time
Book summary
Alikuwa ni mwanamke aliyenifanya niwaache wanawake zangu wote niliokuwa nao ili nibaki na yeye tu. Machoni mwangu alikuwa mrembo zaidi kuliko wanawake wote niliowahi kuwa nao. Masikioni mwangu alikuwa na sauti nzuri zaidi kuliko nilizowahi kuzisikia. Na kikubwa tulishabihiana kwenye vipaji vyetu vya kuimba mziki. Lakini siku tulipokuja kuachana, aliondoka na kila chembe ya hisia ya kupenda tena mwanamke mwengine isipokuwa yeye.