Umilisi wa FASIHI SIMULIZI
Digital ebook. One copy per order, available in your library right after payment.
Fasihi Simulizi ni sanaa inayotumia mazungumzo na vitendo kisanii ili kuwasilisha maarifa au ujumbe fulani kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kwa ujumla, Fasihi Simulizi ni sanaa inayobuniwa kuwasilishwa na kusambazwa kwa (lugha ya) mdomo, na vyombo vyake vikubwa ni mdomo na sauti ya binadamu katika hali ya kuimba, kusimulia, kuiga, kughani, kutamba na kutega kama vile vitendawili vinavyotegwa kwa hadhira. Kuzuka na kukua kwa sayansi na teknolojia kumeathiri pakubwa maana ya Fasihi hii, Fasihi Simulizi ya jamii ijuayo kusoma na kuandika ni tofauti sana na fasihi simulizi ya jamii isiyo na uandishi, kwa vile imeathiriwa na ujuzi wa kusoma na kuandika na mitindo ya masimulizi yake hayaendi sambamba na mitindo ya masimulizi yasiyoathiriwa na uandishi. Hata hivyo, utamu wa Fasihi Simulizi ungali upo.
Book summary
What readers are saying
No reviews yet
Read this book? Share what you thought and help other readers decide.
Write the first reviewReaders also enjoyed