`
Nani Mwanamke? book by Shamte Kilalile

Nani Mwanamke?

Subtitle: Aina 8 Za Wanaume Zinazowavutia Wanawake

Author: Shamte Kilalile

This ebook is selling at KSh. 200 180

Hiki ni kitabu cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vya Nani Mwanamke vyenye lengo la kuelezea saikolojia ya mwanamke katika maamuzi yake hususani mahusiano. Kitabu hiki kinaelezea vipi hisia za mwanamke zinamuongoza katika kijisehemu au kipengele cha uchaguzi wa mwanaume. Yaani vipi hisia zake zinamfanya kuvutiwa zaidi na wanaume aina fulani kuliko wanaume wa aina nyingine. Walengwa wa kitabu hiki ni wanaume na wanawake. Kwa wanaume ni makundi mawili; 1. Kwa wanaotarajia kuoa: watafaidika kuepuka kosa kongwe linalofanywa na wanaume katika mahusiano na kujua sifa mbadala za kujipamba nazo mwanaume ili kumpata mwenza wa Maisha yake. 2. Kwa walio kwenye ndoa: watafaidika kwa kubadilisha tabia au sifa mbaya walizokuwa nazo ili kunusuru ndoa zao. Kwa wanawake; 1. Tafiti zinaonyesha wanawake wengi hawajui kwanini wanavutiwa na wanaume aina hizi. Kwa hiyo kupitia kitabu hiki wanawake wataweza kujua saikolojia yao. 2. Kuwapa wapenzi wao kama njia ya kufikisha ujumbe.

Keywords for this book

Aina 8 Za Wanaume Zinazowavutia Wanawake
Aina 8 Za Wanaume
Wanaume
Wanawake
Kuvutia

You can only order 1 ebook at a time


Book summary

“Aina gani ya mwanaume anayekuvutia?” Ukimuuliza swali hili mwanamke yoyote hutakosa kusikia baadhi ya sifa hizi zifuatazo za mwanaume; 1. Mwenye hofu ya Mungu/Mcha Mungu, 2. Mwenye pesa/Tajiri/anayeweza kunihudumia 3. Mwenye upendo/mapenzi 4. Mwenye kujali 5. Mwenye mvuto/muonekano mzuri 6. Mwenye heshima/sio msaliti Kama utakuwa umesoma kwa makini utagundua kuwa sifa tajwa hapo juu ni baadhi ya sifa za mwanaume bora (good man) na mwenye mamlaka (dominant). Maswali ya kujiuliza ni kuwa, ni kwanini 1. kuna wanawake wanapenda kuwa kwenye mahusiano na wanaume wanaoweza kuwatawala? 2. kuna wanawake wanavutiwa na wanaume ambao licha ya kuwatesa lakini hawaachani nao? 3. kuna wanawake wanapenda wanaume ambao licha ya kujua wanawasaliti lakini hawaachani nao? 4. kuna wanawake ambao wanapenda wanaume wenye muonekano wa kawaida kabisa au wale ambao jamii inawaona wana sura mbaya? Kwanini hali ziko namna hii? Majibu ya maswali haya yako kwenye kitabu hiki.

Write a review

Book details

Publishing date: Oct 5, 2024
Book format: Ebook
Language: Swahili
ISBN 13:
Book size: 1
Cover lamination type: 1
Category: Parenting & Relationships
Total reviews: 0
Total Ratings:
Average Rating: 0 / 5
Other Books by author: SHAMTE KILALILE