Nani Mwanamke?
Subtitle: Aina 6 Za Wanaume Zisizowavutia Wanawake
Author: Shamte Kilalile
Aina 6 Za Wanaume Zisizowavutia Wanawake ni kitabu cha pili kinachoelezea aina za wanaume ambao hawajui kuzigusa hisia za wanawake katika mahusiano hivyo huambulia 'vibuti' au kutodumu kwenye mahusiano yao. Hiki ni katika mfululizo wa vitabu vinavyoelezea saikolojia ya mwanamke katika mahusiano.
Keywords for this book
You can only order 1 ebook at a time
Book summary
Aina 6 Za Wanaume Zisizowavutia Wanawake ni kitabu cha pili katika mfululizo wa vitabu vya Nani Mwanamke ambavyo vinaelezea saikolojia ya mwanamke katika kufanya maamuzi hususani kwenye mahusiano. Kitabu hiki cha pili ni upande mwengine wa shilingi wa wanaume ambao wanazivuruga na hawajui kuzigusa hisia za wanawake. Nimekiandika mahususi kwa ajili ya; 1. Kumuonyesha mwanaume kama hakujiona kwenye kitabu cha kwanza cha Aina 8 Za Wanaume Zinazowavutia Wanawake bila shaka anaweza kuwa kwenye aina hizi kwenye kitabu hiki cha pili. 2. Wanaume ambao huambulia ‘vibuti’ kila wanapotongoza wanawake hivyo hujihisi kuwa hawana bahati. 3. Wanaume ambao hawadumu kwenye mahusiano au ndoa zao. Kila akiwa na mwanamke baada ya muda tu mahusiano au ndoa huvunjika. Kupata majibu ya kwanini hali huwa namna hii, soma kitabu hiki.